Watu maarufu waunga mkono mpango wa UM wa kukabiliana na kifua kikuu

6 Disemba 2011

Mpango mpya ulioanzishwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu ambao hupoteza maisha ya mamilioni ya watu kila mwaka, umepata msukumo mpya kufuatia kundi la watu maarufu kujiunga na mpango huo kwa shabaya ya kutoa elimu zaidi duniani.

Kundi la watu mashuri kutoka nchi za Georgia, Ghana, Jordan, Nepal, Pakistan, Peru, Sudan, Afrika Kusini linatazamia kuunga mkono kampeni zilizoanzishwa na shirika la afya dunia WHO kwa shabaya moja ya kutoa elimu na kwa wananchi namna ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Msukumo mkubwa unaotazamiwa kutiliwa kipaumbele wakati wa kampeni hiyo ni pamoja na kuyamiza mataifa duniani kuongeza ufadhili wa fedha ili kutokomeza kasi ya ugonjwa huo. Katika taarifa yake mwaka huu, WHO ilisema kuwa kwa mara ya kwanza kiwango cha watu wanaougua ugonjwa huo kilipungua lakini ikaonya juu kukosekana kwa vipaumbele vipya ambavyo vinakwazwa kutokana na kukosekana kwa fedha.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter