Walemavu wanastahili kujumuishwa kwenye maendeleo:Ban

2 Disemba 2011
Serikali na wanachama wa mashirika ya umma kote duniani wametakiwa kuanza kuwajumuisha watu walemavu kwenye sekta zote za kimaendeleo. Wito huu umetolewa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye ujumbe wake wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu duniani.

Amesema kuwa kuna changamoto nyingi katika kumaliza umaskini miongoni mwa walemavu na kuwahakikishia ajira na huduma za afya. Ujumbe huu umewasilishwa na naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose-Migiro mjini New York hii leo.

(SAUTI YA ASHA ROSE-MIGIRO)

Nami pia nilipata kuzungumza na mmoja wa walemavu ambaye alinieleza baadhi ya changamoto wanazopitia walemavu.

(MAONI)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter