Waliokufa vita vya Korea waenziwa, na misaada iko matatani:Ban

30 Novemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyataka mataifa yaliyoendelea kutofanya matatizo ya uchumi yanayoikabili dunia hivi sasa kuwa kizingiti cha utoaji wa misaada kwa mataifa masikini. Akizungumza kwenye kongamano la kimataifa la misaada linaloendelea mjini Busan Korea Kusini siku ya Jumatano amesema msaada unasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya watoto, umepunguza kusambaa kwa virusi vya HIV na ukimwi na pia umesaidia kupunguza umasikini uliokithiri duniani kote.

Ban amesema kupunguza misaada hakutosaidia masuala ya bajeti bali kutawaumiza zaidi watu masikini ambao ndio wako katika hatari duniani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezuru makaburi ya Busan Korea ya Kusini siku ya Jumatano ili kutoa heshima zake kwa askari wa kigeni waliokufa wakitetea taifa lake wakati wa vita ya mwaka 1950 hadi 53. Ban amesema anawaheshimu na kuwaenzi mashujaa 2,300 waliopoteza maisha yao katika vita hivyo.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud