Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupunguza gesi chafu ni ajenda kuu kwenye mkutano wa Durban

Kupunguza gesi chafu ni ajenda kuu kwenye mkutano wa Durban

 

Takriban mataifa 200 yamekutana mjini Durban Afrika ya Kusini na kuanza mjadiliano ya kimataifa kuhusu hali ya hewa. Huku muda ukiyoyoma kuokoa mkataba wa Kyoto wenye lengo la kupunguza kiwango cha gesi ya viwandani, wanasayansi wanalaumu kupanda kwa kina cha bahari, vimbunga, ukame na mavuno duni katika kilimo.

Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma ameambia ujumbe katika mkutano huo kwamba ongezeko la joto duniani tayari linasababisha athari na vita barani Afrika. Amesema kuwa watu wengi kwenye nchi zinazoendelea za Afrika mabadiliko ya hali ya hewa ni suala la uhai na kifo.

Mkutano huo wa wiki mbili unatafuta njia za kudhibiti ongezeko la gesi chafu inayoathiri hali ya hewa ambayo wataalamu wanasema imefikia kiwango cha hatari.