Kuikumbusha dunia juu ya mauwaji ya Holocaust kutasaidia kuondoa chuki:UM
Dunia inapaswa kuelezwa na kukumbushwa kwa ufasahu kuhusiana na matukio ya kusikitisha kama mauwaji ya Holocaust ili kuzua matendo kama chuki, uhasama na malumbano. Hayo ni kwa mujibu wa afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa aliyekuwa akizungumza kwenye maadhimisho ya kukumbuka mauwaji ya halaiki yaliyotokea miaka 70 iliyopita nchini Ukraine
Kiyo Akasaka amesema kwa kuikumbusha dunia na kupeleka taarifa sahihi juu ya matukio ya namna hiyo kutasaidia pakubwa kuzua kujitokeza tena kwa hali kama hiyo.
Afisa huyo amesisitiza juu ya kile alichokiita kuendelea kuweka na kutunza kumbukumbu za waathirika wa matukio ya namna hiyo na wakati huo huo kuendelea kuzipa uzito wa pekee kazi na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Umoja wa Mataifa.