Meya wa zamani wa Kivumu Rwanda ahukumiwa na ICTR kwenda jela miaka 15

17 Novemba 2011

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu inayoshughulikia kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda ICTR iliyoko mjini Arusha Tanzania leo imemkuta na hatia meya wa zamani wa Kivumu Kibuye na kumuhukumu kwenda jela miaka 15.

Majaji watatu walioshiriki kwenye hukumu hiyo wanasema Gregorie Ndahimana ana hatia ya kushiriki kwa mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa kusaidia, kuchochea na kwa kutoa amri kwa polisi kwenye eneo la Kivumu.

Majaji wote wamekubaliana kwamba Ndahimana alihusika na uhalifu huo na kifungo cha miaka 15 kitameza hukumu zote alizopewa na isitoshe muda aliokaa kifungoni tangu alipokamatwa Agosti 11 mwaka 2009 utajumuishwa kwenye hukumu hiyo.

Ndahimana alikamatwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kusafirishwa hadi Arusha ICTR Agosti 26 mwaka 2006. Alizaliwa Kivum mwaka 1952.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter