Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Indonesia:Ban asisitiza kupambana na ukataji miti

Indonesia:Ban asisitiza kupambana na ukataji miti

 

Jopo la kimataifa linalohusika na mabadiliko ya hali ya hewa limesisitiza haja ya kimataifa ya kupunguza gesi ya viwandani kushika kasi muongo huu, lakini hata hivyo kiwango cha gesi hiyo kwa mwaka 2010 kimekuwa cha juu katika historia amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akitoa taarifa kwenye nchi Indonesia siku ya Alhamisi. Amesema mpango wa kupunguza gesi itokanayo na ukataji miti na uharibifu wa misitu yaani REDD una lengo la kuzalisha fedha kutokana na gesi ya cabon iliyoko katika misitu.

Mradi huo unatoa fedha kwa nchi zinazoendelea ili kupunguza gesi kutoka katika misitu na kuwekeza katika njia zinazotumia gesi kidogo ya cabon kwa ajili ya maendeleo endelevu. Ban amesema mpango huo wa REDD unaweza kuwa wa mafanikio kwa Indonesia na dunia kwa ujumla.

(SAUTI BAN KI-MOON)