Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za haraka zinahitajika kukabiliana na virusi vinavyotishia mihogo Afrika Mashariki:FAO

Hatua za haraka zinahitajika kukabiliana na virusi vinavyotishia mihogo Afrika Mashariki:FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO imetaka kuchukuliwe hatua za haraka ili kukabiliana na virusi vinavyoshambulia zao la mihogo katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki na kutishia upatikanaji wa zao hilo la chakula katika kanda hiyo.

Ugonjwa wa mihogo uiitwao cassava Brown Streak (CBSD) ni virusi vipya vinavyoathiri hususani nchi za maziwa makuu vinaonekana kuwa tatizo kubwa Afrika Mashariki imesema FAO. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)