UNICEF yashangazwa na kuuawa kwa watoto nchini Somalia

15 Novemba 2011

Mwakilishi wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF nchini Somalia Sikander Khan amesema kuwa kumekuwa na vifo vingi vya watoto wakati kunapoendelea kushuhudiwa mapigano kusini na kati kati mwa Somalia. Kulingana na Umoja wa Mataifa ni kwamba watoto 24 waliuawa kwenye mapigano mwezi Oktoba ikiwa ni mara mbili zaidi ya mauaji yaliyoshuhudiwa miezi ya nyuma.

Watoto wengine 58 wameripotiwa kupata majeraha mabaya mwezi Oktoba ikiwa ndiyo idadi kubwa zaidi ya watoto waliojeruhiwa kwa mwezi mwaka huu. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter