Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washangazwa na kuongezeka kwa ghasia za uchaguzi nchini DRC

UM washangazwa na kuongezeka kwa ghasia za uchaguzi nchini DRC

Kikosi cha kulinda amani kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC kimeelezea kusikitishwa kwake kutokana na kuongezeka kwa visa vya ghasia za uchaguzi na matumizi ya lugha mbaya na viongozi wa kisiasa ambayo imetawala kampeni za urais na za ubunge. MONUSCO inasema kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia matamshi mabaya ya kuwachochea watu kufanya ghasia ikiongeza kuwa huo ni ukiukaji wa sheria za uchaguzi za nchi hiyo.

Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC na mkuu wa kikosi cha MONUSCO Roger Meece ameliambia baraza la Umoja wa Mataifa kuwa MONUSCO na Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa wanatoa usaidizi kwa tume huru ya uchaguzi nchini DRC inapojiandaa kwa uchaguzi utakaofanyika tarehe 28 mwezi huu.