Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulizi la kigaidi lililotokea nchini Nigeria

Ban alaani shambulizi la kigaidi lililotokea nchini Nigeria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani shambulizi la kigaidi lililotokea nchini Nigeria ambapo watu kadha waliuawa na kutaka wahusika kufikishwa mbele ya sheria.

Takriban watu 65 waliuawa kwenye miji iliyo Kaskazini ya Damaturu na Potiskum baaada ya wanamgambo wa kiislamu kushambulia makanisa, misitiki na vituo vya Polisi ambapo pia walipambana kwa muda na vikosi vya polisi. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)