Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la UM lawataka Waliberia kushiriki kwenye uchaguzi

Baraza la Usalama la UM lawataka Waliberia kushiriki kwenye uchaguzi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa wahusika wote kushirikina na kuhakikisha kuwa shughuli ya upigaji kura imeenda shwari nchini Liberia. Hii ni kufuatia ripoti kuwa kumekuwa na madia ya kuwachochea wahusika kususia uchaguzi huo.

Awamu ya pili ya uchaguzi wa urais inatarajiwa kufanyika Jumanne kati ya mshindi wa tuzo la amani Ellen Johnson-Sirleaf na Winston Tubman aliyeibuka wa pili kwenye awamu ya kwanza ya uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 11. Madai yameibuka kuwa bwana Tubman amekataa kushiriki kwenye uchaguzi huo kwa tuhuma kuwa hautafanyika kwa amani. Monica Morara na taarifa kamili.

(SAUTI YA MONICA MORARA)