Watu zaidi wauawa kwenye mapigano eneo la Lower Jubba

4 Novemba 2011

Watu kadhaa wanaripotiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa kufuatia mapigano yanayoendelea kwenye maeneo ya Lower Juba na Middle Juba nchini Somalia. Watu 12 wanaripotiwa kuuawa kwenye eneo la Lower Juba na zaidi ya 70 kujeruhiwa.

Ripoti kutoka wilaya ya Jilib inasema kuwa watu 49 wamejeruhiwa na wengine 10 kuuawa wakiwemo watoto wawili walio chini ya miaka mitano kufuata mashambulizi kwenye mji wa Jilib. Kwa sasa shirika la afya duniani WHO limepeleka vifaa vya matibabu kwenye hospapitali wanakotibiwa majeruhi vitakavyowahudumia watu 10,000 kwa muda wa miezi mitatu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter