Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kutoa misaada kwa waathiriwa wa mafuriko nchini Cambodia

WFP kutoa misaada kwa waathiriwa wa mafuriko nchini Cambodia

Mafuriko makubwa yamewalazimu watu kuhama makwao nchini Cambodia mafuriko ambayo pia yameharibu mazao yao. Mkurugenzi wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP nchini Cambodia anasema kuwa misaada ya chakula inahitajika kwa sasa na siku zijazo wakati watu wanapoendelea kurejea maisha yao ya kawaida na kuongeza kuwa huenda familia maskini zikakosa chakula.

WFP kwa ushirikiano na serikali ya Cambodia na mashirika mengine yasiyokuwa ya serikali imesambaza misaada ya dharura kwa karibu watu 60,000 kwenye sehemu zilizoathirika zaidi.