Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azindua kundi la kusadia kuunga mkono upatikanaji wa nishati kwa wote

Ban azindua kundi la kusadia kuunga mkono upatikanaji wa nishati kwa wote

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametangaza wanachama wa kundi ambalo limetwikwa jukumu la kutafuta mchango wa serikali, mashirika ya kibinafsi na ya umma kwenye jitihada zake za kuhakikisha kuwepo kwa nishati safi na nafuu kwa kila mmoja.

Akihutubia waandishi wa habari mjini New York Ban amesema kuwa kando na masuala ya kubuniwa kwa nafasi za ajira, usalama, afya na hali ya wanawake kawi limesalia suala muhimu kwa kila nchi. Kundi hilo litachangia katika kuweka mikakati ya kuunga mkono lengo la Ban na malengo mengine matatu yanayohitaji kutimizwa ifikapo mwaka 2030.