Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya hali ya hewa ya miongo miwili iliyopita:UNEP

Mabadiliko ya hali ya hewa ya miongo miwili iliyopita:UNEP

Suala la mabadiliko ya hali ya hewa duniani kwa muda wa miaka 20 iliyopita ni kati ya yale yaliyozungumziwa kwenye ripoti mpya ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP iliyotolewa hii leo. Ripoti hiyo inatolewa kama sehemu ya utafiti wa mazingira duniani wa shirika la UNEP.

Katibu Mkuu wa UNEP Achim Steiner amesema kuwa huu ni wakati wa serikali na mashirika ya umma kutoa maoni yao kuhusu jinsi mkutano wa Rio unaweza kuleta mabadiliko ikiwemo kuchangia kwenye maendeleo kwa watu bilioni saba walioko duniani sasa. Waiganjo Njoroge ni afisa wa mawasiliano wa UNEP Nairobi ilikotolewa ripoti hiyo na anafafanua waliyobaini katika ripoti

(SAUTI YA WAIGANJO NJOROGE)

Ameongeza kuwa ripoti kamili ya UNEP itazinduliwa mwezi Mei mwaka ujao mwezi mmoja kabla ya mkutano wa Rio utakaofanyika nchini Brazil.