Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia inaelekea mtafaruku mkubwa wa ajira:ILO

Dunia inaelekea mtafaruku mkubwa wa ajira:ILO

Tathimini iliyotolewa na shirika la kazi duniani ILO katika mkesha wa kuanza kwa mkutano wa viongozi wa G-20 inasema uchumi wa dunia uko katika hatihati ya kutumbukia katika mtafaruku mkubwa wa ukosefu wa ajira.

ILO inasema hali hiyo itachelewesha zaidi kuchipuka upya kwa uchumi baada ya mdororo na huenda ikachochea machafuko zaidi katika nchi mbalimbali.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa taasisi ya kimataifa ya kazi katika shirika la ILO Raymond Torres anasema dunia imefikia wakati wa kumbua ukweli kwamba kuna fursa finyu ya kuepuka tatizo mara mbili la ukosefu wa ajira.

(SAUTI YA RAYMOND TORRES)