Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yatoa wito wa hatua za kuiokoa Niger kutoka kwenye njaa

WFP yatoa wito wa hatua za kuiokoa Niger kutoka kwenye njaa

Hali ya ukosefu wa chakula nchini Niger inaendelea kutia wasiwasi huku ikitarajiwa kuwa mbaya zaidi ikiwa hatua za mapema hazitachukuliwa. Familia nyingi kwa sasa hawana uwezo wa kukabiliana nayo baada ya ya hali kama hiyo kushuhudiwa mwaka mmoja uliopita.

Kulingana na shirika la mpango wa chakula duniani WFP ni kwamba watu milioni moja wanahitaji msaada wa chakula baada ya Niger kupata mazao duni kutokana na ukame ulioikumba nchi hiyo . George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)