Burundi yasema haitavunjika moyo licha ya wanajeshi wake kuuawa Somalia

28 Oktoba 2011

Huko Burundi, Jeshi la nchi hiyo limesema kwamba halitavunjika moyo licha ya tukio la hivi karibuni nchini Somalia ambako walinda amani wake katika kikosi cha Amisom waliuwawa wiki iliopita. Hata hivo giza linaendelea kutanda kuhusu idadi ya wanajeshi waliouwawa.

Taarifa za kutofautiana zilitolewa, Al Shabab wakidai kuwauwa wanajeshi wa Burundi zaidi ya 70 huku Jeshi la Burundi likitangaza idadi ya wanajeshi wasiozidi kumi waliouwawa.

Wiki hii kumefanywa mazishi ya wanajeshi hao mjini Bujumbura katika hali ya usiri mkubwa na hivo kuhoji idadi kamili ya walindamani waliofariki nchini humo.

Burundi imetuma askari Elfu nne nchini Somalia katika kikosi cha Amisom kinachojumuisha pia wanajeshi wa Uganda.

Mkuu wa Majeshi ya Burundi ni Meja Jinerali Godfroid Niyombare.

(SAUTI YA MEJA JENERALI GODFROID NIYOMBARE)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud