Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wawatunuku wanafunzi kutokana na uvumbuzi wao

UM wawatunuku wanafunzi kutokana na uvumbuzi wao

Jiko ndogo ambalo linaweza kutumiwa kwenye mapishi ya nyumbani na linalotumia majani yaliyokaushwa na makaratasi ni kati ya miradi miinne iliyobuniwa na wanafunzi na ambayo inapata tuzo la Umoja wa Mataifa la uvumbuzi wa kimazingira.

Sara Rudianto kutoka Indonesia , Maria Rosa Reyes Acosta kutoka Ecuador , Michael Muli kutoka Kenya na Mary Jade Gabanes kutoka Ufilipino walipokea tuzo hilo kila mmoja kutokana na miradi yao.

Wote hao watapokea pauni 3000 kila mmoja na usaidizi wa kiufundi kwenye nchi zao ili kuiwezesha miradi yao kufanya kazi. Wanne hao waliteuliwa na majaji kutoka shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP.