Wanafunzi wengi hawapati masomo ya shule ya upili Afrika

Wanafunzi wengi hawapati masomo ya shule ya upili Afrika

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa kumekuwa na mahitaji makubwa ya elimu ya shule ya upili ikiongeza kuwa serikali nyingi hususan zilizo kusini mwa jangwa la sahara zina wakati mgumu huku wanafunzi wakiwa hawaendi shuleni.

Kulingana na shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO ni kuwa kuna asilimia 36 tu ya nafasi kwenye shule za upili kwenye nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara. Mkurugenzi wa UNESCO Irina Bokova anasema kuwa hakuna njia ya kuweza kujikwamua kutoka kwenye umaskini bila ya kuwepo elimu ya shule za upili.

Monica Morara na taarifa kamili