Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guatemala, Morocco, Pakistan na Togo zateuliwa wanachama kwenye Baraza la Usalama la UM

Guatemala, Morocco, Pakistan na Togo zateuliwa wanachama kwenye Baraza la Usalama la UM

Guatemala, Morocco, Pakistan na Togo zitakuwa wanachama wasio wa kudumu miongoni mwa wanachama 15 wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 2011-2013 baada ya kushinda viti hivyo kwenye uchaguzi mwishoni mwa juma lililopita kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Wanachama wa Umoja wa Mataifa walipiga kura ya siri kuwachagua wanachama hao watano kuambatana na sehemu za kijiografia watatu wakitoka Afrika na eneo la Asia Pacific, mmoja kutoka Mashariki mwa Ulaya na mmoja kutoka Amerika Kusini na Caribbean.