Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jitihada za kuokoa maisha zaendelea Dadaab

Jitihada za kuokoa maisha zaendelea Dadaab

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR pamoja na washirika wake wanaendelea kuwahudumia maelfu ya wakimbizi kwenye kambi ya Dadaab nchini Kenya. Kunashuhudiwa idadi ndogo ya wakimbizi wanaoingia kwenye kambi hiyo kutoka Somalia suala ambalo huenda limechangiwa na oparesheni za kijeshi zinazoendelea au mvua kubwa inayonyesha.

Zaidi ya wahudumu 30 wa UNHCR bado wanasalia kwenye kambi tatu za Daadab zikiwemo Ifo, Dagahaley na Hagadera sawa na kambi mpya ya Ifo 2 na Kambioos. UNHCR pia inashirikiana na serikali ya Kenya ili kupeleka polisi zaidi kwenye kambi hizo kwa minajili ya kuwahakikishia usalama wakimbizi na watoa huduma. Daadab ndiyo kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani ikiwa na wakimbizi 463,000