Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kubadilishana wafungwa baina ya Israel-Hamas ni hatua nzuri:Ban

Kubadilishana wafungwa baina ya Israel-Hamas ni hatua nzuri:Ban

Tangazo la hivi karibuni la Israel na kundi la Palestina la Hamas la kubadilishana wafungwa ni hatua ya kukaribishwa ambayo itachagiza zaidi juhudi zinazoendelea za kutatua mgogoro wa Mashariki ya Kati amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Israel na Hamas walitangaza wiki iliyopita kwamba wameafikiana kuwa Hamas itamwachilia askari wa Israel Gilad Shalit, ambaye amekuwa akishikiliwa mateka tangu Juni 2006 na Israel itawaachilia zaidi ya wafungwa wa Wapalestina 1000 inaowashikilia. Kwa mujibu wa duru za habari zoezi hili litaanza wiki hii.