Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama wa chakula duniani:UM

Usalama wa chakula duniani:UM

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD na shirika la mpango wa chakula duniani WFP wameungana kuadhimisha siku ya chakula duniani. Siku hii huadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kuchagiza dunia kukabiliana na matatizo ya chakula, kauli mbiu mwaka huu ni “usalama wa chakula kuelekea tulivu”.

Akizungumzia siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mwaka huu ni wa kuelezea kupanda na kushuka kwa bei ya chakula hali ambayo inazidi kuwaweka pabaya masikini ambao wengi hutumia asilimia 80 ya pato lao kwa kununua chakula hali ambayo inasikitisha.

Shirika la FAO limekuwa msitari wa mbele kuchagiza dunia katika kukabiliana na mfumuko wa bei ya chakula. Mkurugenzi wa FAO ni Jacques Diouf

(SAUTI YA JACQUES DIOUF)

FAO ambayo leo pia inaadhimisha mwaka wa 60 tangu kuhamishia makao yake makuu mjini Rome imemtangaza Jeremy Iron mcheza filamu wa Uingereza kuwa balozi wake mwema. Katika hafla maalumu mjini Rome wakuu wa WFP na UN-Women pia wamezungumzia hali ya chakula duniani.