Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe mpya wa UM nchini Iraq akaribishwa nchini humo

Mjumbe mpya wa UM nchini Iraq akaribishwa nchini humo

Mwakilishi maalum mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Martin Kobler amepokewa na waziri mkuu wa nchi hiyo Nuri Ak- Maliki akisema kuwa atashirikiana na utawala nchini Iraq kuisadia nchi hiyo kupiga hatua. Bwana Kobler aliye pia mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq (UNAMI) alimshukuru bwana Al- Maliki kwa mchangao aliotoa kwa ujumbe huo na kundi zima la UM lililo nchini Iraq.

Wakati huo huo shirika la mpango wa chakula duniani WFP nchini Iraq limeadhimisha siku ya chakula duniani kwa kuangazia wajibu wa chakula wakati wa mizozo.