Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua kubwa kulinda idadi ya watu nchini somalia hasa mikoa ya kati na kusini

Hatua kubwa kulinda idadi ya watu nchini somalia hasa mikoa ya kati na kusini

Inakadiriwa kuwa watu millioni 2.5 nchini Somalia, wameathirika na ukame, njaa, na vita. Watu hawa sasa wapo katika athari ya kuambukizwa na ugonjwa wa malaria endapo msimu wa mvua utakapoanza.

Kuzuia vifo vya watu kutokana na ugonjwa huu, hususani watoto wadogo walio na utapiamlo na watu walioathiriwa na vita, hatua thabiti zimeanza kuchukuliwa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Shirika la Afya duniani WHO, na mashirika mengine yameanza kutayarisha hatua za kupambana na malaria endapo ugonjwa huo ukizuka.

Mfuko wa kimataifa wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu na malaria yaani “Global Fund” pamoja na idara ya maendeleo ya kimataifa ya Uingereza yametoa misaada kusaidia utekelezaji wa hatua hizi.

“ Afya ya wasomali imeathirika pakubwa kutokana na ukame, na njaa, hasa watoto walio na utapiomlo. Wakati wa msimu wa mvua ugonjwa wa malaria unaongezeka. Amesema Bw. Sikandar Khan mwakilishi wa UNICEF nchini Somalia.

Pia amesema lazima tuchukuwe hatua haraka iwezekanavyo ili kuokoa maisha ya watu kutokana na ugonjwa huu hatari.