Pillay apongeza kukamilika kwa tathmini ya kwanza ya haki za binadamu kwa mataifa 193

13 Oktoba 2011

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, leo amepongeza Baraza la haki za binadamu kwa kukamilisha tathimini ya hali ya haki za binadamu kwa mataifa yote wanachama 193.

Bi Navi Pillay amesema sasa anatarajia matokeo mazuri kwa mataifa hayo katika kulinda na kuchagiza haki za binadamu. Mchakato huo mpya wa tathimini umekamilika leo ambapo kila taifa mwanachama limefanyiwa tathimini ya hali yake ya rekodi yake ya haki za binadamu katika kipindi cha miaka mine.

Ameongeza kuwa muongo huo mpya umedhihirisha kuwa ni wa ubunifu, wazi na wa ushirikiano katika kufanikisha kuleta mabadiliko kwa nchi zote wanachama wa baraza la haki za binadamu. Pia amesema tathimini hiyo ni fursa muhimu kwa mataifa wanachama kubadilishana zoefu na kushauriana.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud