Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa UM wa kupunguza vifo vya wavuvi kuanza kutumika Septemba ijayo

Mkataba wa UM wa kupunguza vifo vya wavuvi kuanza kutumika Septemba ijayo

Mkataba unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wenye lengo la kupunguza takriban vifo 24,000 vinavyotokea wakati wa shughuli za uvuvi kote duniani unatarajiwa kuanza kutumika mwezi Septemba mwaka ujao ikiwa ni zaidi ya miaka 17 tangu upitishwe na shirika la kimataifa la mabaharia IMO.

Mkataba huo ulipata sahihi yake ya 15 kutoka kwa taifa la Palau tarehe 29 mwezi Septemba na kuweka muda wa miezi 12 wa kuanza kutekelezwa kwake. Usalama wa wavuvi na vyombo vya uvuvi ni kati ya majukumu ya shirika la IMO.