UM walaani shambulio la kujitoa muhanga Moghadishu

4 Oktoba 2011

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Dr Augustine Mahiga amelaani vikali shambulio la bomu la kujitoa muhanga hii leo kwenye ofisi za serikali ya mpito mjini Moghadishu ambalo limekatili maisha ya watu wengi na kujeruhi wengine.

Balozi Mahiga amesema ameshtushwa na kusikitishwa sana kitendo hicho cha kikatili na kisichostahili, amesema mauaji ya raia wasio na hatia hayawezi kkbalika kwa sababu yoyote ile .

Balozi Mahiga ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha na waliojeruhiwa kwenye shambulio hilo la bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari.

Mwezi Agost mwaka huu kuundi la wanamgambo wa Kiislam la Al-Shabaab lilitangaza kujiengua kutoka Moghadishu na vikosi vya serikali ya mpito vikisaidiwa na Muungano wa Afrika sasa ndio vinadhibiti wilaya nyingi za mji mkuu Moghadishu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud