UNHCR na IOM walalamikia hatua ya kutangazwa Lampedusa kuwa eneo lisilo salama

30 Septemba 2011

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na lile la Save the Children ni mashirika yanayoshirikiana kwenye kituo cha Lampedusa wameishutumu serikali ya Italia ya kutangaza bandari ya Lampedusa kuwa isiyo salama.

Mashirika hayo yanasema kuwa tangazo hilo huenda likavuruga shughuli za kuwaokoa wahamiaji na watafuta hifadhi baharini na kuzifanya kuwa ngumu. Mashirika hayo yanalalamika kuwa hatua hiyo huenda pia ikatatiza juhudu za uokozi hasa wakati huu kuna hali mbaya ya hewa na wakati inapolazimu kusafirisha watu kupata matibabu ya dharura pamoja na watoto. Jumbe Omari Jumbe kutoka IOM anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud