Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wamkumbuka na kumuenzi Profesa Wangari Maathai

UM wamkumbuka na kumuenzi Profesa Wangari Maathai

Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mwanamazingira Profesa Wangari Maathai. Shirika la Umoja wa mataifa la mazingira UNEP ambalo Wangari alikuwa mlezi wa kampeni yake ya kupanda miti bilioni moja limesema Profesa Wangari Maathai alikuwa mmoja wa wanakampeni mkubwa wa mazingira duniani na alitambulika kwa kupigania sio mazingira tu bali demokrasia, haki za binadamu na mali asili.

UNEP imesema kifo chake ni pigo kubwa kwa wanamazingira na wote walio mfahamu Maathai kama mama, ndugu, mfanyakazi mwenzao, mfano wa kuigwa na hata kwa waliofurahia azima yake ya kuifanya dunia kuwa mahala pa amani, pa afya na pazuri pa kuishi.

Nalo shirika la chakula na kilimo FAO limeamua kumuenzi Profesa Wangari Maathai alipoteuliwa Februari 2005 kuwa balozi mwema wa mazingira ya msitu wa Congo Basin, ambapo Maathai alisema balozi mwema mmoja hatoshi na kuwataka viongozi wa dunia kumuunga mkono kwa kuchangisha fedha.

(SAUTI YA WANGARI MAATHAI)