Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za visiwa vidogo zaomba usaidizi kutoka nchi zingine ulimwenguni

Nchi za visiwa vidogo zaomba usaidizi kutoka nchi zingine ulimwenguni

Waakilishi wa nchi za visiwa vidogo wameutaka ulimwengu utilie maanani athari zinazokumbana nazo kutokana na kuwepo kwa mabadiliko ya hali ya hewa duniani wakiongeza kuwa hakutakuwa na maendeleo kwa kuwa maji ya bahari yanatishia kuwameza.

Waakilishi hao wanasema kuwa ulimwengu unajikokota katika kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa au katika kuzisaidia nchi maskini kuishi na athari hizo. Waziri mkuu wa Grenada Tillman Thomas ametoa wito wa kuwepo makubaliano kwenye mijadala ya UM ya kupatikana kwa suluhu la gesi zinazochafua mazingira yanayokisiwa kusababisha kuongezeka kwa joto duniani.