Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Liberia itaendelea kuhitaji msaada wa kimataifa hata baada ya uchaguzi mkuu-UM

Liberia itaendelea kuhitaji msaada wa kimataifa hata baada ya uchaguzi mkuu-UM

Katika wakati ambapo uchaguzi mkuu unaotegemewa kufanyika nchini Liberia ukisubiriwa kwa hamu kubwa kwa vile ndiyo utaotoa fursa ya pekee kuimarisha hali ya amani ya nchi hiyo iliyoharibiwa vibaya na vita, hata hivyo bado nchi hiyo italazimika kuendelea kutegemea uungwaji mkono toka jumuiya ya kimataifa.

Kulingana na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika eneo la afrika magharibi, ili kuimarisha hali ya amani na usalama, Liberia inalazimika kutegemea kuungwa mkono na washirika wa kimataifa. Uchaaguzi mkuu wa rais na wabunge uliopangwa kufanyika Oktoba 11 mwaka huu ni uchaguzi wa pili kufanyika tangu kukoma kwa miongo kadhaa ya machafuko na vita.

Akijadilia duru za Liberia, Ellen Margrethe Loj amasema kuwa kama uchaguzi huo wa usoni utafaulu kufanyika kwa mazingira ya amani na uhuru, haitamanisha kwamba sasa kazi ya kusalia kwa vikosi vya kimataifa katika nchi hiyo imemalizika.