Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu milioni 8 Afrika Mashariki wanahitaji chakula:UM

Watu milioni 8 Afrika Mashariki wanahitaji chakula:UM

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa idadi ya watu wanaohitaji misaada ya dharura ya chakula kwenye nchi za Afrika Mashariki imeongezeka kwa watu milioni mbili zaidi hadi watu milioni nane wakati nchi zinapoendelea kushuhudia hali ya ukame.

OCHA inasema kuwa kutokana na hali hiyo mavuno yalipungua, kukawa na uhaba wa maji na malisho na pia mifugo wakafariki nchini Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia na Uganda kutokana na kutokuwepo kwa mvua kati ya mwezi Oktoba na Disemba mwaka uliopita.

Zaidi ya mifugo 5000 wameripotiwa kufariki katika eneo la Marsabit nchini Kenya mwezi Januari mwaka huu wakati zaidi ya wafugaji 10,000 kutoka Somali wakiingia Kenya huku mifugo 30,000 na wafugaji 10,000 kutoka Kenya wakiingia nchini Uganda.