Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS na Marekani watangaza mipango mipya kwa afya ya wanawake

UNAIDS na Marekani watangaza mipango mipya kwa afya ya wanawake

Taasisi ya George W. Bush rais wa zamani wa Marekani, idara ya mambo ya ndani ya Marekani, mfuko wa Rais kwa ajili ya AIDS PEPFAR kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na ukimwi UNAIDS wametangaza mpango wa ushirikiano uitwao utepe wa pink, utepe mwekundu ili kuchagiza sekta za umma na binafsi kusaidia kukabiliana na saratani ya kizazi na ya matiti ambayo ni magonjwa yanayoongoza kwa vifo vya saratani katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na Amerika Kusini.

Mpango huo wa shirikiano utaongeza uwezekano wa watu kupimwa na kupata tiba, na pia elimu ya kutunza matiti hususani kwa wanawake walio katika hatari ya kupata saratani ya kizazi kwenye nchi zinazoendelea kutokana na kuambukizwa virusi vya HIV.  Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)