Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha maafikiano baina ya Sudan kusini na kaskazini kuhusu jimbo la Abyei

Ban akaribisha maafikiano baina ya Sudan kusini na kaskazini kuhusu jimbo la Abyei

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha maafikiano kati ya Sudan Kusini na serikali ya Sudan ya kuondoa majeshi yote kwenye eneo linalozozaniwa la Abyei ambalo kwa mda mrefu limekuwa chachu ya mvutano baina yapande hizo mbili.

Serikali za nchi hizo mbili ziliafikiana mwishoni mwa wiki mjini Addis Ababa Ethiopia katika mazungumzo yaliyowezeshwa na jopo maalumu la muungano wa Afrika linaloongozwa na Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki. Ban amezipongeza serikali hizo mbili kwa muafaka huo ambao unajumuisha kuanzishwa kwa kamati ya pamoja ya kushughulikia suala la Abyei. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)