Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufikiwaji wa amani Darfur ni hatua inayotekelezeka: UM

Ufikiwaji wa amani Darfur ni hatua inayotekelezeka: UM

Kupatikana kwa makubaliano ya usitishaji mapigano na kuwepo kwa mkazo wa kufukiwa kwa amani ya kudumu katika eneo lenye mzozo la Darfur,  ni zingatio muhimu ambalo linapaswa kupewa kipaumbele. Hayo ni kwa mujibu wa Mkuu wa vikosi vya kulinda amani vya kimataifa UNAMID, Bwana Ibrahim  Gambari ambaye pia amezitolea mwito pande zote zinazozozana kuheshimu makubaliano ya amani yaliyofikiwa hivi karibuni.

Amesema makubaliano hayo ya usitishwaji mapigano yaliyofikiwa baina ya serikali na vikundi vya waasi yanapaswa kuheshimiwa na pande zote kwani yanatoa taswira ya maridhiano na maelewano.

Bwana Gambari ambaye anaongoza muungano wa vikosi vya pamoja baina ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika ambaye pia ni mpatanishi kwenye mzozo huo amataka kuwepo kwa utashi uendelevu ili hatimaye yale yaliyokubaliwa yanazingatiwa.