Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran huenda inatengeneza silaha za nyuklia:IAEA

Iran huenda inatengeneza silaha za nyuklia:IAEA

Iran huenda inatengeneza silaha za nyuklia ambazo zinaweza kutumiwa kwa makombora amesema mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA.

Bwana Yukio Amano ameiambia bodi ya magavana ya IAEA mjini Vienna Austria hii leo kwamba Iran haitoi ushirikiano kwa shirika hilo ili kubainisha kwamba haitumii vifaa vya nyuklia kutengeneza silaha.

Kwa upande wake Iran imeendelea kusisitiza kuwa mipango yake ya nyuklia ni ya amani. Hata hivyo bwana Amano amesema shirika lake linatiwa hofu na mipango hiyo.

(SAUTI YA YUKIYA AMANO)