Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zimetakiwa kujizuia kutumia nguvu kupita kiasi kwa watu wao:Pillay

Serikali zimetakiwa kujizuia kutumia nguvu kupita kiasi kwa watu wao:Pillay

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amezitaka serikali na viongozi wanaokabiliwa na kipindi cha mpito kisiasa kujizuia kuwakandamiza raia wao. Bi Navi Pillay amesema watu wote walioko madarakani lazima wachuke hatua kuzia kutekelezwa kwa uhalifu au vitendo vya kulipiza kisasi.

Akizungumza kwenye kikao cha 18 cha baraza la haki za binadamu kilichoanza leo mjini Geneva amesema kuwalinda raia lazima kuwe kitovu cha hatua yoyote itakayochukuliwa na Umoja wa Mataifa katika siku za usoni. Amesema ripoti za kukamatwa na mauaji nchini Libya, na kushikiliwa kwa watetezi wa amani Yemen na Syria ni masuala yanayotia hofu.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

Ameongeza pia kuwa Syria watu takribani 2600 wameuawa hadi sasa tangu kuzuka kwa maandamano ya kutaka demokrasia mwezi Machi.