Mkutano wa UM juu ya kukabili mabadiliko ya tabia nchi kwa mifumo ya teknolojia wamalizika

5 Septemba 2011

Mkutano wa Umoja wa Mataifa uliojumuisha wataalamu wa teknolojia iliyoundwa na umoja huo kwa ajili ya kushughulikia masuala ya tabia nchi umemalizika huku wajumbe wakisema umepiga hatua kubwa.

Umoja wa Mataifa iliunda kamati maalumu ya wataalamu wa teknolojia ili kusaidia kusuma mbele hatua za ufikiaji wa shabaya pamoja kuhusiana na utekelezaji maazimio ya kimataifa yanayoweka zingatia la mazingira.

Wakikutana mjini Bonn, Ujerumani wajumbe kwenye kamati hiyo wameweka mkazo wa matumizi ya mifumo ya teknolojia ili kusaidia kufikia malengo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huo uliodumu kwa muda wa siku tatu pia umejadilia fursa za kubadilishana taarifa na ujuzi na wakati huo huo zikiweka zingatio la namna la kuyashirikisha makundi mbalimbali kwenye mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mkakati huo pia umeweka shabaya ya kuyashirikisha makundi ya wataalamu, wasomi, watafiti pamoja na mashirika mengine ya kiraia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud