Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake ambao uchungu wa kuzaa unaanzishwa wako na hatari ya kupata matatizo ya kiafya: WHO

Wanawake ambao uchungu wa kuzaa unaanzishwa wako na hatari ya kupata matatizo ya kiafya: WHO

Utafiti kutoka kwa shirika la afya duniani WHO unaonyesha kuwa wanawake wajawazito walio na afya wanaweza kuwa kwenye hatari ya kukumbwa na matatizo ya kiafya iwapo uchunguzi wa kuzaa utaanzishwa

[Monica Morara anaripoti]

Uchunguzi huo ulilinganisha uchungu wa kuzaa unaoanzishwa na ule wa kawaida miongoni mwa wanawake 40,000 barani Amerika Kusini. Uchunguzi huo uligundua kuwa wanawake ambao  uchungu wao unaanzishwa bila ya sababu yoyote wako kwenye hatari mara tatu zaidi ya kulazwa  kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kuliko wale wanaosubiri uchungu wa kuzaa wa kawaida. Hata hivyo utafiti huo haukupata hatari yoyote kwa watoto wanaozaliwa na akina mama ambo uchungu wao wa kuzaa unaanzishwa.