Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawaokoa wahamiaji 850 waliokwama Tripoli

IOM yawaokoa wahamiaji 850 waliokwama Tripoli

Meli iliyopelekwa na shirika la kimataifa la wahamiaji IOM kwa ajili ya kuwakwamua wahamiaji waliokwama kwenye maeneo mbalimbali nchini Libya,imefanikiwa kuondoka katika mji mkuu Tripoli ikiwa na wahamiaji 850. Wengi walinusuriwa ni pamoja na raia wa Libya. Makundi mengine ni wanawake na watoto. Meli hiyo hivi inapiga kasi kuelekea katika mji wa Benghazi na inatazamiwa kutia nanga leo usiku.

Ikiwa hapo maafisa wa IOM wanatazamiwa kuwapa huduma za dharura na baadaye baadhi yao watasafirishwa hadi Misri. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)