Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaingilia kati kunusuru afya za wakimbizi wa Somalia

IOM yaingilia kati kunusuru afya za wakimbizi wa Somalia

Wakati kukiripotiwa kuzidi kufumuka magonjwa yanayo waandama wakimbizi wanaokimbia nchini mwao Somalia na kuelekea katika nchi za jirani, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wahamiaji IOM, limetangaza kuanza kusambaza huduma za kitabibu kwa wakimbizi hao.

Shirika hilo likishirikiana na washirika wake, limesema kuwa limelazimika kuingilia kati kusambaza huduma za kiafya ili kunusuru maisha ya wasomalia hao wanaoendelea kukimbilia katika nchi za jirani. Tayari kambi kadhaa zilizoko huko Ethiopia zimekumbwa na magonjwa ya mlipuko na kuna wasiwasi wa kupindukia kwa hali hiyo

IOM imesema kuwa inafanya kazi kwa kushirikiana na wahisani wengine ikiwemo shirika la kuhudumia watoto UNICEF pamoja na mamlaka za serikali za Ethiopia ili kutoa misaada ya dharura ya madawa.