Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Boti ya IOM yawasili Tripoli kusafirisha wahamiaji waliokwama Libya

Boti ya IOM yawasili Tripoli kusafirisha wahamiaji waliokwama Libya

Boti ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM inaelekea mjini Tripoli Libya ili kuwasafirisha wahamiaji waliokwama mjini humo. Boti hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 300 imeondoka kwenye mji wa Mashariki wa Benghazi leo asubuhi baada ya kukamilisha kuwahamisha wahamiaji 124 siku ya Jumapili kutoka Misrata.

Boti hiyo Tasucu itawasili Tripoli Jumanne na itaondoka kuelekea Benghazi baada ya kupakia wahamiaji na kuwapeleka kwenye mpaka wa Misri wa Salloum kabla ya kuwasafirisha hadi makwao. Jumbe Omari Jumbe afisa wa IOM anafafanua zaidi kuhusu operesheni hiyo.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)