Baraza la usalama lataka jitihada zaidi kuleta utengamao Jamhuri ya Afrika ya Kati

19 Agosti 2011

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limetoa mwito likitaka kuchukuliwa na hatua za haraka ili kuleta hali ya utulivu katika nchi ya Jamhuri ya Kati ambayo inakabiliwa na mkwamo wa kisiasa. Baraza hilo la usalama limeitaka ofisi yake inayohusika na ustawi wa eneo hilo UNOCA kuangalia uwezekano kwa kuungana na mashirika mengine ili kukabiliana na hali ya kukosekana kwa usalama ikwemo kuenea kwa wingu kwa silaha pamoja na madawa ya kulevya.

Kundi la kiasi la Lord resistance army LRA limepiga kambi kwenye maeneo kadhaa ya nchi hiyo na kuzuia kitisho cha ukosefu wa amani. Baraza la usalama limesisitiza juu ya haja ya UNOCA kuendelea kufanya kazi bega kwa bega na mashirika mengine ili kuifikisha kwenye kikomo mkwamo huo wa amani.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter