Mwanajeshi wa UNAMID auawa Darfur

5 Agosti 2011

Mwanajeshi mmoja wa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika AU kinacholinda amani kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan UNAMID ameuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya wakati gari lao lililokuwa na wanajeshi watano liliposhambuliwa na watu wasiojulikana katika kijiji cha Duma kilomita 37 kaskazini mashariki mwa nyala kusini mwa Darfur.

Eneo la Darfur limekuwa kwenye mzozo huku kukiwa na mapigano kati ya vikosi vya serikali, makundi yanayoiunga mkono serikali na makundi ya waasi tangu mwaka 2003 ambapo mamilioni ya watu wamekimbia makwao na wengine kulazimishwa kukimbilia nchi majirani. Wanajeshi kutoka UNAMID wametumwa kuchunguza tukio hilo huku aliyehusika kwenye shambulizi hilo akiwa bado hajulikani. Wanajeshi 30 wa kikosi cha UNAMID washauawa tangu kikosi hicho kutumwa kwenye jimbo la Darfur Disemba mwaka 2007.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud