Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unyonyeshaji wa watoto wapunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano

Unyonyeshaji wa watoto wapunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano

Wakati kunaposherehekewa wiki ya kunyonyesha duniani shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limeungana na washirika wake kote duniani likitoa wito wa kutangazwa kwa Umma manufaa ya kumnyonyesha mtoto ili kuhakikisha kuwa vijana kwenye nchi zinazoendelea na zilizostawi wanaelewa umuhimu wa kunyonyesha mtoto kabla hawajakuwa wazazi.

Unyonyeshaji unaaminika kuchangia katika kupunguza vifo vya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano wakati ambapo, ni asilimia 36 tu ya watoto walio chini ya miezi 6 ndio unyonyeshwa kwenye nchi zinazoendelea. Daktari Maria del Carmen Casanovas kutoka shirika la afya duniani WHO amezungumza na radio ya UM kuhusu baadhi ya manufaa ya kumnyonyesha mtoto.

(Sauti ya Daktari Maria del Carmen Casanovas)