Vitendo vya ubakaji vinavyowahusu askari wa kulinda amani vyapungua

28 Julai 2011

Ripoti mpya zilizotolewa kuhusiana na madai ya kuhusika kwenye vitendo vya ubakaji vinavyodaiwa kufanywa na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na nchini Liberia zinaonyesha kupungua kwa zaidi ya asilimia 75.Ripoti hizo zimezingatia kipindi cha kuanzia mwaka 2008. Kupungua kwa matukio hayo kunakuja baada ya kuimarishwa mifumo inayowabana askari wanaotumbukia kwenye matukio korofi

Akijadilia hali hiyo kamanda wa vikosi vya umoja wa mataifa nchini Congo MONUSCO, amesema kuwa bado jitihada zaidi zinaendelea kuchukuliwa ili kudhibiti vitendo hivyo .Chander Prakash, amefahamisha kuwa hata hivyo baadhi ya madai yaliyowaandamana askari hao yalikosa udhibitisho hivyo hakuna hatua zilizochukuliwa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter