Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande zinazozozana Libya haziko tayari kukubaliana- Mjumbe wa UM

Pande zinazozozana Libya haziko tayari kukubaliana- Mjumbe wa UM

Hakuna hatua iliyopigwa kwenye ufikiaji suluhu ya kisiasa nchini Libya wakati pande zote zikiendelea kuhanikiza tofauti zao, tangu pale ilipozuka wimbi jipya la kutaka kuondosha madarakani utawala uliopo. Kwa mujibu wa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la hilo Abdul Ilah Al-Khatib,pande hizo zinazozozana bado zinavutana namna ya ufikiwaji wa suluhu.

Hatua hiyo imekuja baada ya mjumbe huyo kuwa na mazungumzo na pande zote mjini Tripoli na huko Benghazi ambako alijadiliana na pande zote kwa nyakati tofauti.Hata hivyo pande hizo zimeonyesha udhabiti wa kuendelea na majadiliano zaidi yatayoratibiwa na Umoja wa Mataifa